YERUSALEM, Israel
MSEMAJI wa wapiganaji wa Hamas, amesema wataanza kuwaua mateka wanaowashikilia katika Ukanda wa Gaza iwapo Israel itaendelea kulipua makazi ya raia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, amethibitisha zaidi ya watu 100 walichukuliwa mateka. Kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu, lilitishia kumuua mateka wa Israel kila mara Israel inaposhambulia kwa mabomu nyumba ya Wapalestina bila ya onyo, huku Israel ikiwaita askari wa akiba 300,000 ambao hawakuwahi kushuhudiwa na kuweka vizuizi katika Ukanda wa Gaza na kuzusha hofu, ilipanga shambulio la ardhini.
Taarifa kadhaa za televisheni za Israel zilisema idadi ya vifo kutokana na shambulio la Hamas imepanda hadi Waisraeli 900, huku takriban 2,600 wakijeruhiwa, na makumi kadhaa wakichukuliwa mateka.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kulipiza kisasi katika hotuba yake kali akiwashutumu Hamas kwa kuwanyonga watoto waliokuwa wamefungwa na ukatili mwingine.”Adui huyu mbaya alitaka vita na atapata vita” alisema.
Netanyahu alisisitiza kuwa Hamas ijiandae kulipa gharama ambayo `haitasahaulika maishani mwao’ na kwa maadui wote wa Israel, na kwamba “lazima Israel itashinda vita hivyo na ikishinda, basi dunia nzima itashinda.”
BBC.