TAASISI ya kusaidia watu wenye uhitaji Happy Hands Tanzania wahaidi kuendeleza juhudi za kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii wa ndani.
Happy amedhamiria kwa dhati kuunga Mkono juhudi hizo kwa kumleta Mwanamuziki kutoka nchini Sweden, Mahir zein hapa Tanzania na kumpelekea katika Moja ya hifadhi za Wanyama katika Mkoa wa Arusha na Visiwa vya Zanzibar.
Hata hivyo Maher Zein, atakuwepo nchini kwa lengo la kutoa burudani mapema Machi 12 na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kabla ya tarehe rasmi ya Tamasha hilo anatarajiwa kutembelea Mbuga za wanyama zilizopo Arusha.
Aidha, taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imempa nafasi Mwanamuziki huyo kutembelea vivutio vilivyopo Visiwa vya Zanzibar.
Maher zein anatarajiwa kutumbuiza katika Ukumbi wa Dom uliopo Masaki jijini Dar es salaam na kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 50.
Happy ameomba wadhamini kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha Tamasha hilo kwa mwaka huu, kwani mikakati yao ni kuendelea kusaidia wanawake, walemavu pamoja na watoto kwa kiasi kitakachopatikana kupitia Tamasha hilo.
Na AMINA KASHEBA