HALMASHAURI ya jiji la Dodoma imesema haijalitelekeza Soko la Sabasaba maarufu kama soko la mboga mboga na kwamba wanatarajia kulifufua na kulijenga upya na kujenga standi kwa ajili ya mabasi ya daladala ili yaweze kuwa na miundombinu bora na ya kudumu.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ametoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani jijini Dodoma.
Hatua hiyo imekuja kupitia mpango mkakati wa kuboresha mazingira katika jiji la Dodoma pamoja na kuboresha maeneo ya masoko na stendi ya daladala.
“Tunatarajia ifikapo Julai mwaka huu tutaanza ujenzi wa soko la sabasaba na standi kupitia fedha za mradi wa Benki ya Dunia lakini kwasasa tunamwaga kifusi katika stendi hiyo ili kuondoa adha kwa mabasi ya daladala na abiria,”amesisitiza
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya Masoko na stendi ya daladala tayari wameanza kukusanya maoni kutoka kwa wadau ili kuona namna ya kuboresha stendi hiyo na Masoko ya sabasaba, majengo na Makole.
Mafuru amesema kuwa stendi ya sabasa siyo stendi rasimi hivyo kunahitajika uboreshaji Kwa kufumua stendi pamoja sehemu za biashara kwa lengo kubofesha zaidi.
Ameeleza kuwa Soko la sabasaba linatakiwa kufumuliwa lote na kujengwa upya ili liwe na hadhi inayoendana na makao makuu ya nchi.
Na Happiness Mtweve, Dodoma



























