Na Mwandishi Wetu
HALI ya Utulivu, Huzuni na Simanzi imeendelea kutanda nchini huku Watanzania wakiwa katika maombolezo wakimlilia Rais Dk. John Magufuli.
Katika vyombo mbalimbali vya habari nchini vikiwemo Radio na Televisheni, Nyimbo za maombolezo zinaendelea kupigwa ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya siku 14, ambapo Bendera zinapepea Nusu Mlingoti.
Aidha, Salamu za rambirambi kutoka Mataifa mbalimbali zinaendelea kutolewa kwa serikali ya Tanzania kufuatia kifo cha Rais Magufuli, aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam.
Katika Afirika Mashariki, Kiongozi wa kwanza kutoa salamu za rambirambi ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, ambaye ametangaza siku Saba za Maombolezo kwa nchi yake kufuatia kifo hicho.
Salamu nyingine ni kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, pamoja Rais wa Namibia, Hage Geingob.