Idadi ya waliofariki katika tamasha la muziki la Supernova imeongezeka hadi 260, vyombo vya habari vya Israel viliripoti, vikinukuu shirika la uokoaji la eneo hilo Zaka.
Takriban watu 3,000 waliohudhuria tamasha la usiku kucha walilengwa na Hamas kama sehemu ya shambulio kubwa la kushtukiza dhidi ya Israel.
Tamasha hilo lilifanyika katika jangwa la Negev, karibu na Kibbutz Re’im – sio mbali na Ukanda wa Gaza.