YERUSALEMU, Israel
VIKOSI vya Israel, bado vinapambana na wapiganaji wa kundi la Hamas katika maeneo saba hadi nane Kusini
mwa Israel karibu na Ukanda wa Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel limesema Maeneo haya ni pamoja na Be'eri, katika jamii ya wakulima, ambayo yalipenywa na wapiganaji wa Hamas mara moja.
Wengi wa wanamgambo hao wameuawa, lakini wengine bado wamejificha katika nyumba za kibbutz, IDF ilisema
huku Jeshi la Israel likidai kuwa limeshambulia zaidi ya maeneo 1,000 huko Gaza.
BBC.