Fainali ya michuano ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa Wanawake Kanda ya (CECAFA), itachezwa leo katika Uwanja wa Njeru, Uganda kati ya JKT Queens wanaoiwakilisha Tanzania dhidi ya C.B.E ya Ethiopia.
JKT Queens ilikata tiketi ya kwenda fainali baada ya kuichapa Buja Queens ya Burundi mabao 3-1 na kuendeleza rekodi yao nzuri katika michuano hiyo iliyofanyika Uganda huku C.B.E ikitinga fainali kwa kuichapa Vihiga Queens ya Kenya mabao 2-1.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa JKT Queens kushiriki michuano hiyo tangu kuanzishwa mwaka 2021 lakini Tanzania ikiwa mzoefu baada ya mwaka jana Simba Queens kubeba ubingwa huo kwa kuichapa She Cooperate ya Uganda bao 1-0 kwenye fainali.