MKURUGENZI Mkuu wa Jukwaa la huduma kwa njia ya mtandao, Julius Wambogo, amesema kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wanataraji kujenga uchumi wa kijamii na kitaifa kwa kutoa mbinu rahisi za kazi,
Akizungumza Dar es Salaam Wambogo amesema, watashirikiana na watu wenye ubunifu kutekeleza miradi kwa bajeti nafuu.
“Jukwaa la hilo la mtandaoni, hutumia teknolojia ya kidigitali kuwakutanisha watoa huduma na watafuta huduma lengo likiwa ni kubadili mbinu zinazotumika kutafuta na kutoa huduma katika jamii,
Hivyo kupitia teknolojia tumekusudia kubadilisha soko la ajira na utoaji huduma na kuiboresha,hii ni kutokana na athari zilizochangiwa na ugonjwa wa Corona,”amesema Wambogo
Mwambogo amesema kupitia kampuni hiyo ambayo huduma zake hutolewa kupitia jukwaa hilo wakishirikiana sekta binafsi wizara na mataifa ya nje yenye dhumuni ya kukuza uchumi wao, kuimarisha ubunifu na kuondoa umasikini katika jamii.
“Kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo, Wambogo alisema kila mwaka wahitimu 1,000 humaliza masomo yao huku wengine zaidi ya wanafunzi 1,000 wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa fedha.
Pamoja na kwamba wanafunzi hao wanashindwa kuendelea na masomo makampuni mengi huingia sokoni kutafuta wataalamu mbalimbali kila mwaka bila mafanikio,
Utafutaji huu huchukua muda na nguvu ya washiriki kwani uhitaji wa wataalamu unakuwa mkubwa,’’amesema.
Mwambogo amesema kupitia jukwaa la mchongo.com wamekuja na majibu ya changamoto hizo kwa kutoa eneo ambalo wabunifu, watu wenye ujuzi wataonyesha ujuzi wao na kupatikana kwa urahisi na makampuni yenye uhitaji,
Ameongeza kuwa “Tunataraji kuzindua jukwaa hili mwakani na itahusisha watu binafsi ,makampuni miradi ya shirika na ya viwandani katika mtandao wa watoa huduma wenye ujuzi, ubunifu ambao wanautalaamu katika sekta mbalimbali,.
Na MWANDISHI WETU