RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Wallace Karia, amekuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa TFF.
Karia ambaye anagombea kwa mara nyingine kiti hicho, amebaki kuwa mgombea pekee, baada ya wapinzani wake, Hawa Mniga na Evance Mgeusa kukosa vigezo vinavyokidhi kwenda hatua inayofuata.
“Kwa maana hiyo Wallace Karia anasubiri kwenda kuthibitishwa na Mkutano Mkuu na si kumpigia Kura” – amesema Benjamin Kalume, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Na Nasra Kitana