WABUNIFU wa Mavazi hapa nchini wametakiwa kukipa kipaumbele vazi la Kitenge ili kiweze kuinua viwanda vya ndani pamoja na malighafi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam, moja ya wabunifu wanaofanya vizuri katika utayarishaji wa vazi la kitenge nchini, Irfan Riziwanali, amesema kitenge ni moja ya Malighafi inayopendwa na watu wote kutokana na rangi zake pamoja na baadhi ya michoro inayochapishwa.
“Ilinibidi nitengeze vitu mbalimbali kama begi,nguo pamoja na viatu vikiwa na Malighafi ya kitenge kuonyesha kwa jinsi gani nathamini viwanda vya hapa nchini pamoja na utamaduni wa kitanzania wa vazi la kitenge.”
Hata hivyo Riziwanali ameeleza kuwa lengo lake hapo awali lilikua ni kutengeneza mabegi ya kipekee ambayo hapo awali hayakuwahi kubuniwa na mtu yoyote yule.
“Ilinilazimu kushawishi wateja kupenda bidhaa hizo na wateja walivutiwa Sana na bidhaa zetu za mabegi yaliyobuniwa na kitenge na nitaendelea kutengeneza na kubuni vitu kwa kutumia kitenge,” amesema.
Pia amesema kupitia sanaa hiyo ya ubunifu imeweza kumkutanisha na watu mbalimbali nje na ndani ya nchi ambao wamekua msaada katika vitu tofauti tofauti pamoja na kubadilisha mawazo kwa namna gani kazi ya ubunifu itaweza kufika mbali.
Na AMINA KASHEBA