Na JUMANNE GUDE
UZINDUZI wa Kituo cha Kivule Gym Sports & Promotion, kilichopo katika Kata ya Kivule, umeshuhudiwa ukikusanya vijana wengi wakionyesha matamanio ya kudhihirisha vipaji vyao kupitia michezo mbalimbali.
Baadhi ya michezo ambayo vijana hao wa Kivule na maeneo ya jirani wamejitosa ni ngumi, karate, sarakasi na mazingaombwe.
Tukio hilo la uzinduzi lililofanyika leo Juni 21, 2021, limeandaliwa na kituo hicho cha michezo, kwa lengo la kuhamashishavijana wa Kata ya Kivule na maeneo ya jirani kushiriki katika michezo ndani ya maeneo hayo.
Baadhi ya vijana waliojitokeza, wamesema hiyo ni fursa kwao kwa sababu michezo ni ajira na afya.