Wahitimu katika vyuo vya kati Mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia vema fursa na ujuzi wa elimu wanaoupata kuhakikisha wanautumia kujiajiri badala ya kusubiri ajira serikalini.
Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko wakati akizungumza na wahitimu wa fani ya umeme, ufundi wa mitambo na magari chuo cha Veta Matanda.
Meya Masumbuko amesema wengi wa wahitimu husoma kwa kuwa na mawazo ya kuajiriwa serikali na taasisi binafsi jambo ambalo uathiri fikra na mafanikio ya vijana wengi.
“Niwaombe vijana wangu tumieni akili na ufahamu pamoja na ujuzi mlioupata kuhakikisha mnabadili maisha yenu kwa kuutumia vema ikiwemo kujiajiri na kuondoa fikra za kuajiriwa”,amesema.
Masumbuko amewakumbusha wahitimu hao kujiendeleza zaidi kuwa wajuzi wa kitaaluma kwenye fani walizohitimu sambamba na kuondoa dhana ya kuajiriwa.
“Leo Mnahitimu kuna mambo ya kielimu ambayo mmeyapata chuoni hapa hivyo nawashi mkajiendleze huu siyo mwisho bali ni mwanzo wa ufunguo wa maish yenu .
Mnatakiwa kujiamini muondoe ile hofu kile mtakachoenda kukifanya mkifanye kwa kujiamini na siyo kwa kujaribu itakuwa ni busara sana huko muendako kuionyesha heshi
ma hii ambayo mmeondoka nayo hapa kwa wazazi wenu na jamii yote inayowazunguka na kwa muonekano wenu jinsi mnavyojituma, mkifanya kazi kwa bidii katika utendaji wenu watatamani na wengine kuja VTC Matanda”,ameongeza Meya.
Aidha Mstahiki Meya Masumbuko amekitaka Chuo cha Veta Matanda kinachomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Shinyanga kuendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza udahili kwa kuwa chuo hicho kina uwezo wa kubeba wanafunzi zaidi ya 500.
Mstahiki Meya Masumbuko amewataka vijana wa Manispaa ya Shinyanga kutumia vema fulsa za uwepo wa vyuo vya veta katika Manispaa hiyo ikiwemo Veta Matanda, kupata ujuzi ili kuendana na mabadiliko yw teknolojia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Veta Matanda Joaster Kisanko amesema kuwa chuo hicho kimefanikiwa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ukarabati wa madarasa pamoja nambweni.
“Chuo cha Matanda VTC kina historia kubwa tangu kuasisiwa kwake mwaka 1989 na marehemu Askofu wa jimbo katoliki Shinyanga Mhashamu Castory Sekwa aliyekuwa na maono makubwa”,amesema.
Kisanko amesema kwa mwaka huu 2022 jumla ya vijana 10 wamehitimu mafunzo mablimbali ikiwemo fani ya umeme, ufundi magari ambapo ujuzi waliopata utakwenda kuwa msaada kwao.
Mkuu chuo hicho amesema kuwa tangu kuanza upya kwa chuo hicho mwak 2018 kinatoa fani mbalimbali ikiwemo fani ya Umeme,Makenika,Ushonaji, Uashi, Uungaji Vyuma pamoja na Udereva ambapo amesema kwa sasa wana uwezo wa kupokea wananfunzi 540 amesema Kisanko
Mkuu huyo wa chuo amesema kuwa kwa mwaka 2021 mafunzo mbalimbali yalitolewa ikiwemo wahitimu 97 wa udereva, 8 makenika, 5 Ushonaji, 12 Umeme, 2Uungaji Vyuma pamoja kozi ya computer wahitimu 14.
Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa ujuzi waliopata utakwenda kuwa msaada kwao kwa kubadili maisha yao ikiwemo kujiajiri nankutanua wigo wa ajira kwa vijana wenzao.
Chuo cha ufundi Matanda VTC kilianzishwa mwaka 1989 na aliyekuwa askofu wa jimbo katoliki Shinyanga Mhashamu Castory Sekwa kwa kutoa fani mbalimbali zilizolenga kuwainua na kuwajenga vijana ambapo baadae kilifungwa na serikali kwa kukosa sifa mnano mwaka 2018 chuo hicho kimekidhi vigezo na kuanza kutoa mafunzo katika fani mbalimbali.