MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole uliopo Addis Ababa, Ethiopia na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano.
Makamu wa Rais yupo nchini Ethiopia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 5 na 6 Februari 2022.