TIMU ya Manchester United imetupwa nje ya michuano ya yote ya Ulaya baada ya kuchapwa bao 1-0 na Bayern Munich katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana.Bao pekee la Bayern Munich lilifungwa na winga Mfaransa, Kingsley Coman dakika ya 70 na kwa ushindi huo mabingwa wa Ujerumani wanafikisha pointi 16 kileleni, wakati Manchester United inabaki na pointi zake nne mkiani.
FC Copenhagen iliyoshuka 1-0 nyumbani, Sweden jana dhidi ya Galatasaray ya Uturuki inamaliza na pointi zake nane na inafuzu Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Galatasaray iliyomaliza na pointi tano nafasi ya tatu inakwenda UEFA Europa League.