Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Wizara ya Madini kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya madini imeanza maandalizi ya kushiriki maonesho makubwa ya madini Barani Afrika ya Mining Indaba.
Maonesho hayo yatakayofanyika Februari, mwakani katika Jiji la Cape Town, Afrika Kusini na kushirikisha wafanyabiashara, watoa huduma, taasisi mbalimbali za kisekta pamoja na wakuu wa kampuni kubwa za uchimbaji madini duniani.
Akizungumza wakati akiwasilisha mpango wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo kwa Waziri wa Madini kwa niaba ya sekretarieti ya maandalizi, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi Mhandisi Philbert Rweyemamu, alisema ni moja ya maonesho ambayo huwakutanisha wawekezaji wapatao 900, taasisi za sekta zipatazo 40 na
watendaji wa kampuni wapatao 1,000.