Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya mbegu Tanzania unafanyikaleo Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe.
Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo wadau wa Tasnia ya mbegu ni Hali ya Tasnia ya mbegu na mpango wa uendelezaji mbegu, Majukumu ya SAGCOT katika kuwezesha upatikanaji wa mbegu za mazao ya biashara na viazimviringo na Mikakati ya kuwezesha upatikanaji wa mbegu za awali za mazao mbalimbali.
Mada zingine ni fursa za biashara ya mbegu Bora” za mazao ya Kilimo , uthibiti wa ubora wa mbegu,fursa za ajira za wanawake na vijana kupitia Tasnia ya mbegu, upatikanaji wa mbegu Bora” za mazao ya mbogamboga na Miche Bora” ya miti ya matumda na mada ya kujengea uwezo wazalishaji mbegu kupitia BBT.
Baada ya Majadiliano wadau hao watatoka na maazimio ya pamoja lengo likiwa yale watakayokubaliana yatatekelezwa.