YAOUNDE, Cameroon
WATU wengi wanahofiwa kupotea katika Mji Mkuu waCameroon, Yaoundé, baada ya maporomoko ya ardhi
kuharibu nyumba kadhaa katika mtaa wa Mbankolo.
Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika jiji hilo juzi jioni.Hata hivyo, haijulikani idadi ya watu waliopoteza maisha na wengine wengi walipoteza maisha ambapo Novemba, mwaka jana, maporomoko ya ardhi katika mji huo mkuu, yaliua takriban watu 14 waliokuwa wakihudhuria mazishi.
BBC.