WASHINGTON, Marekani
NDEGE ya kwanza iliyobeba zana za kijeshi za Marekan,i imewasili hivi karibuni katika Kambi ya Nevatim Kusini mwa Israel kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo.
“Ushirikiano kati ya wanajeshi wetu, ni sehemu muhimu ya kuhakikisha usalama wa kikanda na
utulivu wakati wa vita,” Jeshi la Ulinzi la Israel, lilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kundi la washambuliaji la USS Gerald R Ford, pia limewasili Mashariki mwa Mediteranian.
BBC.