WANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchuchuma, Wilayani Ludewa mkoani Njombe, wameiomba serikali kuiangalia shule yao kwa jicho la huruma ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Mmoja wa wazazi wa watoto hao, ameiambia UhuruOnline, kuwa matumaini yao makubwa wanayaweka kwa Mbunge wa jimbo hilo, Joseph Kamonga, waliyemtaja kuwa makini katika kushughulikia changamoto za wananchi wake.
Kufuatia kauli hiyo, Mbunge Kamonga ameahidi kufanya jambo kwenye shule hiyo, baada ya kuitembelea hivi karibuni na kujionea mazingira magumu yanayoizunguka jamii ya shule hiyo.
Walimu wa shule hiyo wamewaomba wadau wa wilaya ya Ludewa na wapenda maendeleo, kujitokeza kukarabati madarasa ya shule hiyo badala ya kutegemea juhudi za mbunge pekee, hasa ikizingatiwa ana majukumu mengi.
Na Michael Katona



























