Na Mwandishi Wetu
SERIKALI inatarajia kujenga meli mpya ya mizigo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Karema iliyopo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi pamoja na kujenga barabara ya kiwango cha lami na reli ili kuwezesha bandari hiyo kufanya kazi kwa uwezo wake wote.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alitoa kauli hiyo alipotembelea bandari hiyo jana Tutajenga meli hiyo ili uwekezaji wa serikali wa Sh. bilioni 47.9 ulete tija, ni lazima ipatikane meli kubwa ya mizigo sambamba na ujenzi wa barabara ya lami na reli ya urefu wa kilomita 110 kutoka Mpanda hadi Karema, alisema.