Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa hundi yenye thamani Shilingi Milioni 15 kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaogua Saratani wanaopatiwa matibabu hispitalini hapo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno amesema leo tumekuja hapa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ambapo tuna kongamano letu linalofanyika kila mwaka na tumekuwa tunafanya mambo mengi ikiwa ni kurudisha kwa jamii ambapo mwaka huu tumeamua kwa tusaidie kidogo kwa kuonesha mfano kwa watoto wanaoangaika na Saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweza kuchangia.
Maneno amewasisitiza wadau kushiriki katika kutoa msaada kwa wagonjwa ikiwa ni hali ya kurudisha kwa jamii ambapo leo Bodi ya NBAA imeamua kuja kuoa msaada wa Waasibu na Wakaguzi wa Hesabu walioutoa ikiwa ni kurudisha kwa jamii ili kuweza kukuza huduma za kijamii.
Pia amewashukuru wafanyakazi wote wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa kuendelea kutoa huduma pamoja na kuendelea kufanya maboresho katika hospitali hiyo ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea hasa kwenye Afya kwa kuwa na vifaa bora.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi ameishukuru Bodi ya NBAA kwa kuweza kuwatanisha Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kuja na wazo la kusaidia watoto wenye magonjwa wa Kansa wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amewaomba wadau wengine kuweza kuwasaidia watoto hao pamoja na wangonjwa mbalimbali katika Hospitali hiyo.
“Matibabu ni ghali lakini tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwakuweza kuja nawazo la Bima ya Afya kwa wote ambapo mpaka sasa Bunge limeweza kupitisha Sera hiyo ambapo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwenye suala zima la Matibabu.” Alisema Dkt. Magandi.





























