
Katika mazungumzo hayo Viongozi hao wamejadili namna bora ya kushirikiana ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za Shehena zinazoingia na kutoka Nchini.
Bw. Chen ameambatana na watendaji waandamizi wa kampuni hiyo na kutembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma Bandarini, ameahidi kuendeleza ushirikiano na TPA ili Wateja wao kupata huduma kwa haraka.




