MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Paul Kirigini ameonyeshwa kukerwa na tabia ya viongozi wanaotokana na chama hicho kulumbana hadharani.
Mjumbe huyo wa NEC ametoa rai hiyo leo Alhamisi Agosti 19, jijini Dodoma ambapo amesema malumbano baina ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima na Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, na kuwataka waache mara moja.
Amesema jambo la msingi ni kuangalia namna gani wanatekeleza ilani ya chama hicho kila mtu kwenye ele lake.
ìJambo hili linakera sana kuona kwamba wana-CCM wamefikia sehemu kila mtu anavutia upande wake, huyu hiviÖ yule vile, wanapaswa kuweka tofauti zao pembeni na kujikita katika kusimamia ilani ya Chama.
“Waziri ni msaidizi wa rais anapaswa kutambua dhamana na jukumu kubwa la kumsaidia katika sekta inayomhusu kwa kuzingatia vita kubwa uliyoko mbele yetu ya ugonjwa wa covid-19 zaidi ya kujikita kuelimisha jamii Waziri hapaswi kuingiza malumbano kama sehemu ya kuelimisha Jamii,” amesema Kirigini.
Ameongeza kuwa ugonjwa wowote ni sayansi, tabibu na elimu vinginevyo tunaondoa umakini wa vita iliyoko mbele yetu huku akimtaka mbunge wa Kawe kuacha kauli kinzani.
ìKwa upande wa mbunge wa Kawe namshauri kuacha mara moja kauli kinzani na kuheshimu hatua mbali mbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita kulinda afya za Tanzania.
ìNapenda Watanzania wafahamu suala la Afya ni kipaumbele kwa serikali, tunawataka viongonzi hawa wawili waache mara moja marumbano yasio na tija, kama lipo jambo la kifamilia limalizwe kwa misingi hiyo, vinginevyo kama chama hatutasita kutawachukulia hatua za kinidhamu.
ìTunawasihi viongozi wa aina hii kumpa nafasi ya utulivu Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan katika kushughulikia matatizo ya wa Tanzania kwa ujumla,î amesema Kirigini.