MTANZANIA ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sanaa na utamaduni (Kukaye moto culture center), Arba Manillah, amezawadia tuzo ya Amani katika Mji wa kihistoria wa Chemnitz nchini Ujerumani.
Arba Manillah ni mzaliwa wa Iringa amekuwa akiendelea kuutangaza utamaduni wa Tanzania kwa muda mrefu nchini Ujerumani kwa kupitia, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Kukaye Moto Culture Center.
Akizungumza na UhuruOnline, Manillah amesema tuzo hiyo itakuwa chachu ya kuongeza bidii katika kutangaza utamaduni wa Tanzania.
“Nashukuru kwa kutunukiwa tuzo hii ya Amani, pia nitahakikisha naendelea kutangaza utamaduni wetu huku Ujerumani kupitia sanaa,” amesema Manillah.
Manillah ameeleza sababu ya kufanya kazi nchini humo ni kutanua wigo wa wasanii wa Tanzania kutangaza vipaji vyao na kutangaza vivutio vya utalii, ndiyo sababu ya kutunukiwa tuzo hiyo.
“ Shukrani zangu za dhati kwa serikali ya Tanzania, familia yangu na viongozi wenzangu wakina Antje,Thomas, Andrea, Yvone kwa sapoti na nashukuru Taasisi yangu ya Kukaye Moto Culture Center.” amesema.
Na AMINA KASHEBA