Na Mwandishi Wetu
MTANZANIA Prudencia Paul Kimiti, ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Malkia Elizabeth II kutokana na
mchango wake mkubwa kwenye masuala ya jamii katika hafla iliyoongozwa na binti Mfalme Anne
katika kasri la Windsor, nchini Uingereza.
Prudencia alikabidhiwa Tuzo ya Heshima maarufu kama (MBE) na Mfalme Charles III. Tuzo hiyo ilitokana na mchango wa binti huyo wa Kitanzania katika masuala ya jamii hasa watu weusi na watu wanaotoka Bara la Asia waishio nchini Uingereza.
Prudencia kwa sasa anaishi nchini Uingereza na anafanya kazi kama Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi cha Mamlaka ya Mapato ambapo anahusika na mambo ya forodha na usalama wa mipaka ya Uingereza.Yeye pia ni mwanaharakati wa watu weusi.