Mwanajeshi wa Israel ameuawa wakati wa uvamizi wa ndani huko Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema.
Wanajeshi wengine watatu wa IDF walijeruhiwa – mmoja kwa wastani na wawili kidogo – katika shambulio hilo, alisema msemaji Daniel Hagari kwenye mtandao wa kijamii.
Hagari alisema wanajeshi walikuwa wakitafuta Waisraeli waliopotea na kusafisha eneo hilo wakati shambulio lilipotokea.
“Kombora lilirushwa kwenye kifaru wakati wa uvamizi wa ndani uliofanywa mapema leo katika Ukanda wa Gaza, katika eneo la Kissuf,” aliandika.
Haijulikani ni wapi hasa aliuawa. Eneo la Kissuf liko kwenye mpaka wa Gaza, na gazeti la Times of Israel linasema ilitokea upande wa magharibi wa uzio wa mpaka, ndani ya Gaza.