BAADA ya kumaliza ratiba yake katika Wilaya ya Ukerewe, Mwenge wa Uhuru umewasili jijini Mwanza na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngamagana Amina Makilagi.
Kwa mujibu wa DC Makilagi,ukiwa wilayani humo, mwenge huo utakimbizwa Kilomta 40.7 ambapo utazindua, kutembea na kukagua miradi 9 ya maendeleo yanye thamani ya sh. bilioni 8.1.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Josephine Mwambashi, amesema Mwenge wa Uhuru mwaka huu, unaozunguka nchini na kauli mbiu: “Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji.
Josephine amesema mbio hizo maalumu kwa mwaka huu, pia zinaendelea kusisitiza mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi chini ya kauli mbiu mshikamano wa kitaifa tuwajibike kwa pamoja janga la ukimwi linaendelea kuwa kubwa.
“Katika jamii zetu kuna waathitika wa ugonjwa wa ukimwi hivyo tusiwatenge na tuzidi kuwapatia elimu ya kufika katika vituo vya kupatiwa tiba na dawa za kufubaza maambukizi hayo,” amesema.
Pia amesisitiza wananchi kuendelea na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na kwa hiari, ili kutambua afya zao na kujua namna ya kuishi na hali husika.
Na Johari Shani



























