Na REHEMA MOHAMED
UPANDE wa mashitaka, unatarajia kumsomea hoja za awali msanii wa maigizo Bulton Mwemba ‘Mwijaku’, katika kesi ya kusambaza picha za utupu mtandaoni, hoja zitakazosomwa Machi 24, mwaka huu.
Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu.
Wakili wa serikali, Kija Luzungana alidai kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kumsomea hoja za awali mshitakiwa lakini bado hazijakamilika.
Alidai upelelezi wa kesi hiyo tayari umeshakamilika hivyo aliomba ipangwe tarehe nyingine ya kumsomea mshitakiwa huyo hoja.
Baada ya maelezo hayo, hakimu alikubali ombi hilo na kuipanga Machi 24, mwaka huu.
Mwijaku anakabiliwa na kesi ya kusambaza picha za utupu mtandaoani kinyume cha sheria.
Ilidaiwa kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo katika terehe tofauti kati ya Septemba 17, hadi Oktoba 10, 2019 jijini Da r es Salaam.
Ilidaiwa kuwa, katika tarehe hizo. alisambaza picha za utupu akitumia kompyuta yake kupitia mtandao wa WhatsApp.