Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imetangaza matokeo ya mitihani ya 98 iliyofanyika mwezi Novemba ya Bodi ambapo takwimu zinaonesha watahiniwa 6711 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ufaulu ni asilimia 66.6
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema Ufaulu umepungua kutoka asilimia 67 mpaka 66.6 ambapo watahaniwa 527 hawakuweza kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali, hivyo idadi ya watahaniwa 6711 sawa na asilimia 92.7 walifanya mitihani ambapo wanawake walikuwa 3636 sawa na asilimia 50.2 na wanaume 3602 sawa na asilimia 48.8
Pia Bodi hiyo imezindua mihutasari mipya pamoja na vitabu vya rejea ambapo Bodi ya NBAA hufanya mapitio ya mtaala yake pamoja na vitabu kila baada ya miaka mitano.
Maneno amesema Bodi ilianza mchakato wa kupitia mitaala yake pamoja na vitabu rejea kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022 na zoezi hili lilianza kwa kufanya marekebisho ya Mtaala na baadae zoezi la kupitia vitabu rejea lilifanyika.
“Bodi inaendelea kuboresha mitaala ya kufundishia ili kuongeza idadi ya Wahasibu na Wakaguzi hapa nchini ili kuweza kuchangia katika maendeleo hasa kuhakikisha Hesabu tunazozitoa zinakuwa ni sahihi na zinaaminika.” akisema Maneno
Pia CPA MAneno amesema Bodi itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za elimu ili kuhakikisha maadili yanazingatiwa ili vijana waandaliwe tangu wakiwa vyuoni.
