KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi, amesema katika oparesheni iliyofanyika hivi karibuni kwenye kijiji cha Mituguri, Wilayani Nachingwea, jeshi hilo limekamata meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 11 na bangi yenye uzito wa kilogramu 319.
Akizungumza na wanahabari katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Nachingwea, Kamanda Kitinkwi amesema, mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa ni mwanaume (53),ambaye amekutwa na viroba 18 vya bangi nyumbani kwake.
Kitinkwi amesema kuhusu meno ya tembo, wamewakamata watuhumiwa watatu wanaume Wilayani Liwale, katika kijiji cha Nambinda, wakiwa na meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilogramu 11 na pikipiki aina ya San LG yenye namba za usajili MC 120 BWW.
Kamanda huyo amewaomba wananchi wa Mkoa wa Lindi, kuendelea kulipa ushirikiano mzuri jeshi la polisi pindi linapokuwa katika oparesheni zake, ili vitendo vya kihalifu viondoke katika mkoa huo.
Na Sophia Nyalusi



























