Na Thabit Madai, Zanzibar.
GARI ya Waandishi wa Habari waliokuwa katika Msfara wa Mkamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Sueiman Abdul, imepata ajali katika eneo la Mtule Wilaya ya Kusini wakati wakielekea katika Ziara ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika Ajali hiyo jumla ya watu wanne (4) wamejeruhiwa vibaya huku mwandishi mmoja anaejulikana kwa jina la Khamis Ali Khamis (64) amefariki hapo hapo huku majeruhi wa ajali hiyo wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Majeruhi hao ni Kassim Abdi Hassan (35) Abdulrahim Khamis Mussa(25) Hassan Issa Mwadini (59) Abdullah Khamis Ali (30) Abdulwahid Suleiman Yussuf (26)
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa Tatu na Nusu asubuhi ambapo ajali hiyo ilihusisha gari Nne, mbili zikiwa za binafsi na gari mbili za Serikali ambazo zilikuwa katika msafara huo.
“Gari Nne 4 zimehusika katika ajali hiyo ambapo gari aina ya Alphad iliyokuwa inatokea Shamba kwenda Mjini iliingilia msafara huo wa Makamu wa Pili wa Rais na kusababisha gari mbili prado ambazo zilikuwa k msafara huo kupata ajali pamoja na gari aina ya Rava Z 178 KT ambayo ilikuwa inaendeshwa na mgeni raia wa Romania Salina Flava miaka 24,” Kamanda Suleiman Hassan
Kamanda amesema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya kutokea kwa jail hiyo huku maejeruhi wote wakiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mazi Mmoja Mjini Unguja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdul, amelipongeza juhudi zilizochukuliwa na Madaktari katika hospitali ya Mnazi mmoja katika kuwapoke na kuwahudumia majeruhi wa ajali hiyo.
“Imenibidi kusitisha ziara yangu katika Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kutokea kwa ajali hii ambapo tunawaombea kwa mungu wapone haraka, wale ambao wameata majeraha pia Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi alietutangulia mbele ya haki,” Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdul
Majeruhi wa ajali hiyo wamefikishwa katika hospitli ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu zaidi ambapo Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi wamefika katika hospitali hiyo kuwapa pole majeruhi kuwakagua majeruhi wa ajali hiyo.