Tuesday, March 17, 2026
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

RAIS SAMIA ASHUSHA NEEMA KWA WASTAAFU

admin by admin
December 23, 2021
in Habari Kitaifa
0 0
0
RAIS SAMIA ASHUSHA NEEMA KWA WASTAAFU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
391
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

SERIKALI imeupatia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), sh.trilioni 2.17 ikiwa ni malipo ya awamu ya kwanza ya deni la wastaafu walioanza kazi kabla ya Julai, mwaka 1999, kupitia utaratibu wa hati fungani maalumu kwa ajili ya kuuwezesha mfuko huo kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na kuongeza mapato yake.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wa Wizara ya Fedha, Emmanuel Tutuba, alipozungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano na PSSSF ya ulipaji wa kiasi hicho cha fedha ili kuuwezesha mfuko huo kuboresha utendaji wao wa kulipa mafao kwa wastaafu.

Makubaliano hayo yalifanyika kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali,Tutuba na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Tutuba alisema serikali imeamua kutoa dhamana hiyo baada ya deni hilo kusababisha hitilafu katika mizania ya rasilimali za mfuko huo ikilinganishwa na wajibu wa ulipaji mafao, kwa kuwa mfuko huo umekuwa ukifanya malipo kwa kuzingatia kipindi chote cha ajira ya mstaafu kikiwemo kipindi cha kabla ya Julai 1999 cha kuanzishwa kwa mfuko huo.

“PSSSF ilianzishwa kufuatia kuunganishwa kwa mifuko minne (4) ya Pensheni, ukiwemo mfuko wa PSPF ambao ulianzishwa mwaka 1999 na kuanza kulipa mafao mwaka 2004 kwa kuzingatia kipindi chote cha ajira ya mstaafu kikiwemo kipindi cha kabla ya Julai 1999, maana yake mstaafu wa mwaka 2004 aliyeajiriwa mwaka 1970, alilipwa na mfuko kipindi chote cha ajira yake”, alifafanua.

Alisema kulikuwa na makubaliano na serikali wakati wa uanzishaji wa Mfuko wa PSPF na kwa kuzingatia utaratibu wa kisheria kabla ya mwaka 1999.

Katibu Mkuu huyo alisema serikali imeona ni sahihi kufanya malipo hayo kwa nia njema ya kuhakikisha sekta hiyo muhimu inaendelea kuhudumia Watanzania na kushiriki vyema kwenye ujenzi wa uchumi.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya Shilingi trilioni 2.17 na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, jijini Dodoma.

AGIZO LA RAIS SAMIA

Tutuba alisema kukamilika kwa mpango huo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha ucheleweshwaji wa mafao ya wastaafu wa PSSSF, linafanyiwa kazi kwa haraka ili punde mtumishi anapostaafu apatiwe mafao yake na mwezi unaofuata aanze kupokea pesheni yake ya kila mwezi.

Alisema serikali ina matumaini makubwa kuwa, fedha hizo zilizotolewa zitasaidia katika kulipa mafao ya wanachama wanaostaafu kwa wakati, kuendelea kulipa pensheni za mwezi kwa wastaafu na kutumika katika uwekezaji wenye tija ambao utasaidia kukuza thamani ya mfuko.

Katibu Mkuu huyo aliutaka mfuko huo kuongeza ufanisi na kuhakikisha unawafikia wanachama wake wote nchini hususani wale waliopo vijijini na maeneo yasiyofikika kwa urahisi, ili wanufaike na huduma.

Tutuba alibainisha kwamba, PSSSF imekuwa na deni ililolirithi  baada ya iliyokuwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuvunjwa na kubaki na mfuko mmoja wa watumishi wa umma, hivyo serikali kuamua kulipa deni hilo.

“Kama wizara tumekuwa na majadiliano mara kadhaa na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na sasa PSSSF kuhusu  kushughulikia suala la deni la ‘pre 1999’, baada ya kufanya uchambuzi wa kina wa suala hilo na kwa maslahi mapana ya wanachama wa mfuko.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, wakisaini hati ya makubaliano ya Shilingi trilioni 2.17 kwa ajili ya kuwalipa wastaafu, baada ya kusainiwa, jijini Dodoma.

“Serikali imeamua kulipa deni hilo kwa kuanzia na sh.  trilioni 2.17 na litalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalumu ya kuanzia miaka minane hadi 25,”alisema Tutuba.

Alisema kutokana na makubaliano hayo, anaamini ufanisi na utendaji wa mfuko utaongezeka hususan katika kuwahudumia wanachama ambao wengi sasa wamestaafu.

Katibu Mkuu huyo alisema PSPF  ilikuwa ikiomba serikali kuiongezea uwezo ili ilipe kiinua mgongo na pensheni za mwezi kwa watumishi wa umma ambao walikuwepo katika ajira kabla ya mwaka 1999.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wizara inaamini fedha hizo zitasaidia kulipa mafao kwa wakati ya wanachama wao wanaostaafu, kuendelea kulipa kwa wakati pensheni za mwezi kwa wastaafu na pale zitakapotumika katika uwekezaji  uwe wenye tija, ambao utasaidia kukuza thamani ya mfuko na kutimiza wajibu wao kwa muda mrefu ujao.

“Mpaka sasa serikali imeshailipa PSSSF sh. bilioni 500 kati ya sh. bilioni 724 za deni lililohakikiwa na inaendelea kulipa deni hili,lengo likiwa ni kuona mfuko huo na sekta ya hifadhi ya jamii kunakuwa na ustawi unaotakiwa na hatimaye kulinda maslahi ya wadau kwa muda mrefu ujao,”alisema.

Tutuba alisisitiza  azma ya serikali chini ya Rais Samia ni kuona wastaafu ambao wamelitumikia taifa lao wanafurahia maisha yao ya kustaafu.

Alisema baada ya kutia saini makubaliano yao ni matarajio yao kuwa,malalamiko kutoka kwa wanachama hususan wastaafu yatapungua kwa kiasi kikubwa, kama siyo kumalizika kabisa, huku akiwataka kuendelea kujipanga vema na kwamba wizara ina imani na utendaji wao wa kazi.

Katibu huyo aliuagiza mfuko wa PSSSF kuendelea kuboresha huduma na kuwafikia wanachama waliopo vijijini ili nao wafurahie ustaafu wao popote walipo, badala ya kuwaacha waendelee kufunga safari mpaka makao makuu ya mkoa kwa kutafuta huduma za mfuko.

KASHIMBA

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Kashimba aliishukuru serikali kwa kushughulikia suala la michango ambayo haikuwasilishwa kwa uliokuwa Mfuko wa PSPF kwa jina maarufu la “Pre 1999 liability”.

“Tunakuhakikishia kuwa kila kiasi tutakachopokea kitaelekezwa katika  maeneo kusudiwa, yakiwemo ya uwekezaji ili kuongeza thamani na ukwasi wa mfuko, lakini pia jukumu kuu la ulipaji wa mafao kwa wakati kwa wanachama wetu wanaostahili kulipwa,” alisema.

Akizungumzia historia ya mfuko huo, Kashimba alisema PSSSF ilianzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma Na. 2 ya Mwaka 2018, kufuatia kuunganishwa kwa mifuko ya Pensheni wa LAPF, PPF, GEPF na PSPF ambapo, baada ya kuanzishwa kwake ulirithi mali na madeni yote ya mifuko iliyounganishwa.

Na Happiness Mtweve,Dodoma

admin

admin

Stay Connected test

  • 138 Follower
  • 205k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0

Fire Joker Tragamonedas Juego tragamonedas Kronos Sin cargo En internet

March 17, 2026

Superiores Casinos En internet 2026 Hace el trabajo En Camino joviales Recursos Dolphins Pearl Deluxe sin depósito giros gratis Real

March 17, 2026

Eye of Horus verbunden: Jetzt gratis zum besten geben & Maklercourtage starburst Online -Slot sichern!

March 17, 2026

96 31% RTP, 10.000x Max Win roman legion $ 1 Kaution Demonstration & Echtgeld

March 17, 2026

Recent News

Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 13
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • casino online
  • Casino UK
  • casino utan svensk licens
  • casino1
  • casino4
  • climatica.org.uk
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • Gry
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • News
  • Nos partenaires
  • Online Kasyno
  • Post
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • S Post
  • SIASA
  • Spinathlon
  • Sports
  • test
  • Uncategorized
  • www.kuss.cl

Recent News

Fire Joker Tragamonedas Juego tragamonedas Kronos Sin cargo En internet

March 17, 2026

Superiores Casinos En internet 2026 Hace el trabajo En Camino joviales Recursos Dolphins Pearl Deluxe sin depósito giros gratis Real

March 17, 2026

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In