Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Mhe. Rais ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms) na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Wajumbe wa Tume walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
I. Prof. Florens Luoga – Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;
II. Prof. Mussa Juma Assad Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;
III. Bw. Leonard Mususa – Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania;
IV. CPA. Aboubakar Mohamed Aboubakar Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU);
V.Balozi Mwanaidi Sinare Maajar – Mshauri wa Masuala ya Sheria;
VI. Bw. David Tarimo – Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kodi, PwC;
VII. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi – Katibu Mkuu Mstaafu; na
VIII. Bw. Rished Bade Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).