Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana 5 Novemba, 2023, amkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli ikiwa ni ishara ya kukabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Dkt. John Pombe Magufuli iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria.






























