Na MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amewashauri walimu kukopa kwa malengo ya kuboresha maisha ya sasa na baadaye na kuhakikisha mikopo wanayochukuwa wanaitumia kuanzisha miradi yenye tija.
Ameyasema hayo Dar es Salaam, wakati akifungua Semina ya Siku ya Walimu, iliyoandaliwa na benki ya NMB.
Mkuu huyo wa mkoa, amewataka walimu kuacha kurubuniwa kwa mikopo ya haraka, yenye riba kubwa, ambayo mwisho inawaingiza Katika maisha magumu.
Ametumia fursa hiyo kuwaeleza walimu kuwa namna bora ya kutumia mshahara ni kutumia kidogo na kuweka akiba ya kuanzishia miradi ya kujiimarisha kiuchumi.





























