SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, imezindua mfumo maalumu wa kielectroniki wa kuratibu na kufuatilia shughuli za serikali kwa kukusanya taarifa za utekelezaji katika mipango kazi yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema mfumo huo walianza kuutengeneza tangu mwaka 2017 na mpaka sasa hivi wamefanya juhudi kubwa katika kuuboresha ili uweze kutumika katika kuratibu taarifa na utekelezaji wa mipango na sera za wizara husika.
amesema ziko baadhi ya sera zilizotungwa tangu mwaka 1992 na bado mpaka sasa hazijafanyiwa mikakati yoyote hivyo amewaomba watendaji wote wa wizara, kuhakikisha wanasimamia sera zote ambazo walizitunga na kushindwa kuzifanyia tathimini.
Pia amewataka kuwasilisha taarifa za utekelezaji ili zihifadhiwe kwenye mfumo huo wa kieletroniki.
“Tumeamua kufanya jambo hili ili watanzania waweze kufuatilia mipango mikakati na utekelezaji wa serikali kupitia Wizara zao na nasikitishwa sana na baadhi ya wizara kuto kuleta taarifa zao mpaka sasa hivi ili ziingizwe kwenye mfumo maalumu”. amesema Waziri Muhagama
Na. Benedict Mwasapi, Dodoma



























