Monday, August 4, 2025
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo MICHEZO-MAKALA

SIMBA NA YANGA NI KUFA AU KUPONA

admin by admin
July 3, 2021
in MICHEZO-MAKALA
0 0
0
SIMBA NA YANGA NI KUFA AU KUPONA
0
SHARES
340
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

LEO unaweza kusema ni kufa au kupona, awali ilikuwa ni mwezi, wiki, siku, saa na sasa zimebaki dakika kumaliza tambo za mashabiki wao wa Simba na Yanga.

Mchezo wa leo wa Ligi Kuu mzunguko wa pili, umepangwa kuanza majira ya saa 11 jioni  ambapo presha ya mashabiki na macho itatua ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam  kujua nani ataibuka mbabe baada ya kuwepo tambo nyingi.

Timu hizo, zinachuana leo katika pambano la ligi ya Tanzania Bara inayoshirikisha timu 18.

Filimbi katika mpambano huo, itapulizwa na mwamuzi Emmanuel Mwandembwa   kutoka mkoani Arusha baada ya dakika 90 ndio atajulikana nani mbabe huku atakayefungwa wanachama, wapenzi wake watalala mapema kutokana na kipigo hicho ndani ya dakika hizo.

Mwandembwa atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Hamdani Said kutoka Mtwara wakati mwamuzi msaidizi atakuwa ni Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa mwisho wa wababe hao wa soka nchini walipopambana, Novemba 7, mwaka jana, timu hizo zilitoka uwanjani, zikifungana bao 1-1.

Mwamuzi msaidizi, Frank Komba wa Dar es Salaam, yeye atakuwa anachezesha mpambano huo kwa  mara ya pili mfululizo baada ya kuwepo katika mchezo wa matokeo  ya sare ya kufungana bao 1-1.

Hadi leo hii, Simba ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 73 baada ya kushuka dimbani mara 29 ikiwa imeshinda mechi 23, imetoka sare mara nne  na imepoteza michezo miwili.

Yanga wao wameshuka dimbani mara 31, wameshinda mechi 19, wametoka sare mara 10, wamepoteza michezo miwili na wana pointi zao 67.

Simba imefungwa mabao 12 wakati Yanga wao wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 21  katika michuano hiyo ya ligi ya msimu huu.

Lakini ngome ya Simba imeonekana kuwa ngumu kuruhusu mabao kufungwa  katika wavu wao kuliko Yanga.

UFUNDI

Kuelekea pambano la leo hii, kazi ipo kwenye sehemu za ulinzi, viungo na ushambuliaji kwa timu hizo ambapo watakuwa na jukumu zito kuamua mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa safu ya kiungo ya Simba ipo vizuri na imekuwa chachu ya mafanikio ya timu hiyo msimu huu kwa kutoa pasi safi za kupachika mabao.

Ukiangalia kwenye mechi kadhaa zilizopita, Simba imeweza kupachika mabao 69 wakati Yanga wao wamefanikiwa kufunga mabao 49 hadi leo kwenye ligi hiyo.

Ufundi wa Hassan Dilunga, Clatous Chama na Thadeo Lwanga   kwa upande wa Simba utaongeza ushindani mkali.

Kwa upande wa Yanga,  sehemu ya kiungo inaweza kuwa na Haruna Niyonzima na Tuisila Kisinda wafanye kazi ya ziada.

Timu hizo mbili zitawakosa viungo Jonas Mkude wa Simba na Yanga, itamkosa Carlos Carlinhos ambaye ameondoka katika timu hiyo na kurudi nyumbani kwao nchini Angola.

Simba imekuwa inatumia zaidi mfumo wa kujaza  viungo wengi na kusababisha timu yao kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la timu pinzani huku wakijilinda ili kupata matokeo mazuri.

Ukiacha Mukoko Tonombe, Niyonzima wapo viungo wenye kazi kubwa leo kama watapewa jukumu ndani ya uwanja kuhakikisha ‘mnyama’ hatoki.

Viungo hao watakuwa na jukumu la kuwathibiti wapinzani wao wa Simba ambao wamekuwa bora zaidi hivi sasa licha ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanawalisha mipira washambuliaji wa Yanga wakiwemo Ditram Nchimbi, Said Ntibazonkiza, Michael Sarpong na Yacouba Sogne.

Viungo wa Simba watakuwa na kazi ya kusukuma mipira mbele kwa Meddie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu na Luis Miquissone maarufu ‘Konde Boy’.

MAKOCHA

Katika mpambano wa leo, Yanga itakuwa chini ya Nabi Nasroddine wakati Simba wao watakuwa chini ya kocha Didier Gomes.

KAGERE, BOCCO KUMPIGA KIKUMBO DUBE?

Wakati homa ya mchezo wa watani wa jadi ikizidi kupanda, washambuliaji Meddie Kagere na John Bocco watakuwa na kazi nyingine.

Kazi hiyo ni kutaka kumpiku Prince Dube wa Azam FC, katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu katika michuano hiyo.

Dube ana mabao 14 sawa na Bocco wakati Kagere ana mabao 11, Chris Mugalu ana mabao 10 hadi leo kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

UTAMU UPO HAPA

Ikiwa leo mchezo huo utapigwa, utakuwa wa 106 kwa timu hizo kukutana katika michuano  ya ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

AHADI ZA FEDHA

Wakati mchezo huo unapigwa leo, tayari viongozi wa kila upande wametoa ahadi nono kwa wachezaji wao endapo wataibuka na ushindi leo.

Kwa upande wa Yanga, kampuni ya GSM inayoidhamini klabu hiyo imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuwapa  hamasa nyota wa timu hiyo.

Simba wao wakiahidi kuwapa kila mchezaji  fedha nyingi endapo watailaza Yanga katika mchezo wa leo na kusababisha kuongeza ushindani katika kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Lengo ni kuhakikisha wanakuwa fiti kabla ya kucheza tena na Yanga katika mchezo wa Fainali ya Kombe la FA.

SIMBA WANACHONGA, YANGA KIMYA KIMYA

Wakati mchezo huo ukipigwa leo, viongozi wote wa klabu mbili wameibuka na mitindo miwili tofauti kuelekea mchezo huo.

Yanga wao kupitia kwa Ofisa Habari wao, Hassan Bumbuli na Mhamasishaji wao, Anthony Nugaz wamekuwa  wakizungumza kidogo tofauti na msemaji wa watani wao wa jadi Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara hivi karibuni aliibuka na kuwataka wanachama na wapenzi wa timu hiyo kufika kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao ili kuwasambaratisha Yanga.

Alisema kuwa ana imani asilimia 100 Simba ipo vizuri na wataanza leo ili waweze kupata ushindi wa mabao matatu katika mchezo huo.

Kufuatia hali hiyo, inaonekana viongozi wa Simba wamekuja na staili ya kusema huku wakimnyatia mtani wao wa jadi kwa kauli nzito kwa ajili ya leo kuichapa Yanga.

MAMBO MUHIMU YASIYOSAHAULIKA

Wakati timu hizo, zinashuka dimbani leo, bado timu hizo zimekutana mara 105 katika michuano ya Ligi Kuu.

Katika mechi hizo, yapo baadhi ya mambo ambayo kamwe hayawezi kusahaulika kwa mashabiki wa timu hizo.

Mnamo Machi 3, mwaka 1969 wakati huo Simba ilijulikana kwa jina la Sunderland, iligoma kuingia uwanjani na Yanga ilipewa pointi za chee na ushindi wa mabao 2-0.

Mara ya pili, Simba ilirudia tena kitendo kama hicho, ilikuwa  Agosti 10, mwaka 1985 ambapo Simba waligomea mechi Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam, Yanga ikapewa ushindi wa mabao 2-0.

Lakini Yanga bado ina machungu baada ya Julai  19, mwaka 1977 ilipochapwa mabao 6-0 na Simba

Rekodi hiyo hadi leo hii, haijavunjwa, ingawa Yanga waliwahi kuichapa Simba mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa Juni Mosi, mwaka 1968.

Lakini rekodi nyingine imeingia tena mwaka huu, Mei 8,2021 baada ya mchezo kati ya watani hao wa jadi,kuhairishwa  kufuatia Yanga kugoma kucheza saa 1.00 usiku badala ya saa 11.00 jioni kufuatia kutolewa mabadiliko muda mchache kabla ya mchezo huo kuanza.

Swali linakuja, nani kuibuka kidedea leo katika mchezo huo wa watani wa jadi?

MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA ZA WATANI WA JADI;

JUNI 7, 1965

Yanga v Sunderland (Simba)

1-0

MFUNGAJI: Mawazo Shomvi dk. 15).

JUNI 3, 1966

Yanga v Sunderland (Simba)

3-2

WAFUNGAJI:

Yanga: Abdulrahman Lukongo dk. 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk. 83. Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk. 86.

NOVEMBA 26, 1966

Sunderland v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Mustafa Choteka dk. 44.

MACHI 30, 1968

Yanga v Sunderland

1-0

MFUNGAJI: Kitwana Manara dk. 28.

JUNI 1, 1968

Yanga v Sunderland

5-0

WAFUNGAJI:

Maulid Dilunga dk. 18 (penalti), Dilunga dk. 43, Salehe Zimbwe dk. 54, Zimbwe dk. 89, Kitwana Manara dk. 86.

MACHI 3, 1969

Yanga v Sunderland

(Yanga ilipewa pointi za chee na ushindi wa mabao 2-0, baada ya Sunderland kugoma kuingia uwanjani).

JUNI 4, 1972

Yanga v Sunderland

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Kitwana Manara dk. 19,

Sunderland: Willy Mwaijibe dk. 11.

JUNI 18, 1972

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Leonard Chitete.

JUNI 23, 1973

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Haidari Abeid ‘Muchacho’ dk. 68.

AGOSTI 10, 1974

Yanga v Simba

2-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Gibson Sembuli dk. 87, Sunday Manara dk. 97.

Simba: Adam Sabu dk. 16.

(Mechi ya kihistoria iliyochezwa Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza).

JULAI 19, 1977

Simba v Yanga

6-0

WAFUNGAJI:

Abdallah Kibadeni dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan ‘Masimenti’ dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20.

OKTOBA 7, 1979

Simba v Yanga

3-1

WAFUNGAJI:

Simba: Nico Njohole dk. 3, Mohammed Bakari ‘Tall’ dk. 38, Abbas Dilunga dk.72. Yanga: Rashidi Hanzuruni dk. 4.

OKTOBA 4, 1980

Simba v Yanga

3-0

WAFUNGAJI: Abdallah Mwinyimkuu dk. 29, Thuwein Ally dk. 82, Nico Njohole dk. 83.

SEPTEMBA 5, 1981

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Juma Hassan Mkambi dk. 42

APRILI 29, 1982

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Rashid Hanzuruni dk 2.

SEPTEMBA 18, 1982

Yanga 3-0 Simba

WAFUNGAJI:

Omar Hussein dk. 2 na 85, Makumbi Juma dk. 62.

FEBRUARI 10, 1983

Yanga v Simba.

0-0

APRILI 16, 1983

Yanga v Simba

3-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Charles Mkwasa dk21, Makumbi Juma dk38, Omar Hussein dk84,

Simba; Kihwelo Mussa dk14.

SEPTEMBA 10, 1983,

Yanga v Simba

2-0

WAFUNGAJI: Lila Shomari alijifunga dk. 72, Ahmed Amasha dk. 89.

SEPTEMBA 25, 1983

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Makumbi Juma dk. 75,

Simba: Sunday Juma dk. 72.

MACHI 10, 1984

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Omar Hussein dk. 72.

Simba: Idd Pazi kwa penalti dk 20.

JULAI 14, 1984

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Abeid Mziba dk. 39.

Simba: Zamoyoni Mogella dk. 17

MEI 19, 1985

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Omar Hussein dk. 6

Simba: Mohammed Bob Chopa dk. 30.

AGOSTI 10, 1985

Yanga v Simba

(Simba waligomea mechi Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam, Yanga ikapewa ushindi wa mabao 2-0)

MACHI 15, 1986

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Abeid Mziba dk. 44

Simba: John Hassan Douglas dk. 20.

AGOSTI 23, 1986

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Edward Chumila dk. 9, Malota Soma dk. 51

Yanga: Omar Hussein dk. 5.

JUNI 27, 1987

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Edgar ‘Fongo’ Mwafongo dk. 36.

AGOSTI 15, 1987

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Abeid Mziba dk. 14.

APRILI 30, 1988

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Justin Mtekere dk. 28

Simba: Edward Chumila dk. 25.

JULAI 23, 1988

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Edward Chumila 21, John Makelele dk. 58

Yanga: Issa Athumani dk. 36.

JANUARI 28, 1989

Yanga v Simba

2-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Issa Athumani dk. 4, Abeid Mziba dk. 85

Simba: Malota Soma dk. 30.

MEI 21, 1989

Yanga v Simba

0-0

MEI 26, 1990

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Mavumbi Omari dk 6.

OKTOBA 20, 1990

Yanga v Simba

3-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Makumbi Juma dk 33, Thomas Kipese dk. 82, Sanifu Lazaro dk. 89

Simba: Edward Chumila dk. 58.

MEI 18, 1991

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Said Sued ‘Scud’ dk. 7.

AGOSTI 31, 1991

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Said Sued Scud.

OKTOBA 9, 1991

Yanga v Simba

2-0

WAFUNGAJI: Athumani China dk. 3, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ dk54.

NOVEMBA 13, 1991

Yanga v Simba

(Simba waligomea mechi kipindi cha pili Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam, Yanga ikapewa ushindi wa 2-0)

APRILI 12, 1992

Yanga 1-0 Simba

MFUNGAJI: Kenneth Mkapa dk. 10.

SEPTEMBA 26, 1992

Simba v Yanga

2-0

OKTOBA 27, 1992

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Damian Morisho Kimti.

MACHI 27, 1993

Yanga v Simba

2-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Said Mwamba Kizota dk. 47 na 57

Simba: Edward Chumila dk. 75.

JULAI 17, 1993

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Dua Said dk. 69.

SEPTEMBA 26, 1993

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Dua Said dk. 13.

NOVEMBA 6, 1993

Simba v Yanga

0-0

FEBRUARI 26, 1994

Yanga v Simba

2-0

MFUNGAJI: Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ na James Tungaraza ‘Boli Zozo’.

JULAI 2, 1994

Simba v Yanga

4-1

WAFUNGAJI:

Simba: George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani, Dua Saidi Yanga; Constantine Kimanda.

NOVEMBA 2, 1994

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Madaraka Selemani dk. 71

NOVEMBA 21, 1994

Simba v Yanga

2-0

WAFUNGAJI: George Lucas dk. 18, Madaraka Selemani dk. 42.

MACHI 18, 1995

Simba v Yanga

0-0

OKTOBA 4, 1995

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Said Mwamba ‘Kizota’ dk. 70, Mchunga Bakari dk. 79,

Yanga: Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ dk. 40.

FEBRUARI 25, 1996

Yanga v Simba

2-0

SEPTEMBA 21, 1996

Yanga v Simba

0-0

OKTOBA 23, 1996

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ dk. 46

NOVEMBA 9, 1996

Yanga v Simba

4-4

WAFUNGAJI:

Yanga: Edibilly Lunyamila (penalti) dk. 28, Mustafa Hozza alijifunga dk 64, Said Mwamba ‘Kizota’ dk. 70, Sanifu Lazaro dk. 75.

Simba: Thomas Kipese dk. 7, Ahmed Mwinyimkuu dk. 43, Dua Saidi dk. 60 na 90.

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)

APRILI 26, 1997

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Idelfonce Amlima dk. 16

Simba: Abdallah Msamba sekunde ya. 56

AGOSTI 31, 1997

Yanga v Simba

0-0

OKTOBA 11, 1997

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Sekilojo Chambua dk. 52

Simba: George Masatu dk. 89

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya)

NOVEMBA 8, 1997

Yanga v Simba

1-0

MFUNGAJI: Sekilojo Chambua dk. 85

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma)

FEBRUARI 21, 1998

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Akida Makunda dk. 46

Simba: Athumani Machepe dk. 88

JUNI 7, 1998

Yanga v Simba

1-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Idelfonce Amlima dk. 28

Simba: Abuu Juma (penalti) dk. 32

MEI 1, 1999

Yanga v Simba

3-1

WAFUNGAJI:

Yanga: Idd Moshi dk. 59, Kalimangonga Ongala dk. 64, Salvatory Edward dk. 70, Simba: Juma Amir dk. 12.

AGOSTI 29, 1999

Yanga v Simba

2-0

WAFUNGAJI: Bakari Malima dk. 49, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ dk 71

JUNI 25, 2000

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Steven Mapunda dk. 59 na 72

Yanga: Idd Moshi dk. 4.

AGOSTI 5, 2000

Yanga v Simba

2-0

MFUNGAJI: Iddi Moshi 37 na 47. (Alifunga mabao hayo, akitoka kwenye fungate ya ndoa yake)

SEPTEMBA 1, 2001

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Joseph Kaniki dk. 76

SEPTEMBA 30, 2001

Simba v Yanga

1-1

WAFUNGAJI:

Simba: Joseph Kaniki dk. 65,

Yanga: Sekilojo Chambua dk. 86

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza)

AGOSTI 18, 2002

Simba v Yanga

1-1

WAFUNGAJI:

Simba: Madaraka Selemani 65

Yanga: Sekilojo Chambua (penalti). dk. 89

NOVEMBA 10, 2002

Simba v Yanga

0-0

SEPTEMBA 28, 2003

Simba v Yanga

2-2

WAFUNGAJI:

Simba: Emmanuel Gabriel dk. 27 na 36

Yanga: Kudra Omary dk. 42, Heri Morris dk. 55

NOVEMBA 2, 2003

Simba v Yanga

0-0

AGOSTI 7, 2004

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Shaaban Kisiga dk. 64, Ulimboka Mwakingwe dk. 76

Yanga: Pitchou Kongo dk. 48

SEPTEMBA 18, 2004

Simba v Yanga

1-0

MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk. 82

APRILI 17, 2005

Simba v Yanga

2-1

WAFUNGAJI:

Simba: Nurdin Msiga dk. 44, Athumani Machupa dk. 64,

Yanga: Aaron Nyanda dk. 39

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

AGOSTI 21, 2005

Simba v Yanga

2-0

MFUNGAJI: Nico Nyagawa dk. 22 na 56

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)

MACHI 26, 2006

Simba v Yanga.

0-0

OKTOBA 29, 2006

Simba v Yanga

0-0

JULAI 8, 2007

Simba v Yanga

1-1 (dakika 120)

WAFUNGAJI:

Simba: Moses Odhiambo (penalti dk. 2)

Yanga: Said Maulid (dk. 55).

(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo).

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

OKTOBA 24, 2007:

Simba Vs Yanga

1-0

Mfungaji: Ulimboka Mwakingwe

(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

APRILI 27, 2008:

Simba Vs Yanga

0-0

OKT 26, 2008

Yanga Vs Simba

1-0

MFUNGAJI: Ben Mwalala dk15.

(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

APRILI 19, 2009

Simba Vs Yanga

2-2

WAFUNGAJI:

SIMBA: Ramadhan Chombo dk 23, Haruna Moshi dk 62

YANGA: Ben Mwalala dk48, Jerry Tegete dk90

(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

(Matokeo haya yanahusu mechi za Ligi ya Bara na iliyokuwa Ligi ya Muungano pekee)

OKTOBA 31, 2009

Simba Vs Yanga

1-0

MFUNGAJI: Mussa Hassan Mgosi dk 26

(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

APRILI 18, 2010

Simba Vs Yanga

4-3

WAFUNGAJI:

SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+

YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89

OKTOBA 16, 2010:

Yanga Vs Simba

1-0

MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70

MACHI 5, 2011

Simba Vs Yanga

1-1

WAFUNGAJI:

YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.

SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.

(Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja)

OKTOBA 29, 2011

Yanga 1-0 Simba

MFUNGAJI: Davies Mwape dakika ya 75

MEI 6, 2012

Simba 5-0 Yanga SC

WAFUNGAJI:

Emmanuel Okwi (dk 2 na 62), Felix Sunzu (penalti 56), Juma Kaseja (penalti dk 67) na Patrick Mafisango (penalti dk 72)

(Ligi Kuu)

OKTOBA 3, 2013

Simba 1-1 Yanga SC

WAFUNGAJI:

Simba SC: Amri Kiemba dk3

Yanga SC: Said Bahanuzi dk65

(Ligi Kuu)

MEI 18, 2013

Yanga 2-0 Simba SC

WAFUNGAJI: Didier Kavumbangu dk 5 na Hamisi Kiiza dk 62.

OKTOBA 20, 2013

Yanga SC 3-3 Simba SC

WAFUNGAJI:

Yanga SC: Mrisho Ngassa dk15, Hamisi Kiiza dk36 na 45

Simba SC: Betram Mombeki dk54, Joseph Owino dk58 na Gilbert Kaze dk85.

APRILI 19, 2014

Simba SC 1-1 Yanga SC

WAFUNGAJI:

Simba SC; Haroun Chanongo dk76

Yanga SC: Simon Msuva dk86

OKTOBA 18, 2014

Simba SC 0-0 Yanga SC

MACHI 8, 2015

Simba 1-0 Yanga SC

MFUNGAJI; Emmanuel Okwi dk52

SEPTEMBA 26, 2015

Yanga SC 2-0 Simba SC

WAFUNGAJI:

Yanga SC: Amissi Tambwe dk44 na Malimi Busungu dk79

FEBRUARI 20, 2016

Yanga SC 2-0 Simba SC

WAFUNGAJI:

Donald Ngoma dk39 na Amissi Tambwe dk72

OKTOBA 1, 2016

Simba 1-1 Yanga

WAFUNGAJI:

Yanga: Amissi Tambwe dk26

Simba: Shiza Kichuya dk87

FEBRUARI 26, 2017

Simba 2-1 Yanga

WAFUNGAJI:

YANGA: Simon Msuva (penalti) dk5

SIMBA: Laudit Mavugo dk66 na Shiza Kichuya dk81

 

2020

Yanga 1-0

MFUNGAJI:

Bernard Morrison

NOVEMBA 7,2020

Simba 1 Yanga 1

Wafungaji ni Michael Sarpong kwa upande wa Yanga na Joash Onyango

 

MEI 8,2021

Mechi iliahirishwa na haikuchezwa hadi leo baada ya Yanga kugoma kucheza saa 1.00 usiku badala ya kuchezwa saa 11.00 jioni.

Na MWANDISHI WETU

admin

admin

Stay Connected test

  • 139 Follower
  • 205k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0

Exploring Herbal Viagra Alternatives: Natural Solutions for Men’s Health

May 23, 2025
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

November 11, 2024

Recent News

Exploring Herbal Viagra Alternatives: Natural Solutions for Men’s Health

May 23, 2025
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

November 11, 2024
Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 231
  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Sports
  • Uncategorized

Recent News

Exploring Herbal Viagra Alternatives: Natural Solutions for Men’s Health

May 23, 2025
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In