Simba Sc wameondoka nchini leo alfajiri Desemba 1, 2023 kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya kuwakabili Jwaneng Galaxy, mchezo wao wa pili wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.
Orodha kamili ya wachezaji waliosafiri chini ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha ni hii hapa:
Magolikipa: Ayoub Lakred, Ally Salim na Hussein Abel
Mabeki: Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Fondo Malone, Henock Inonga, Kennedy Juma, Israel Mwenda na Hussein Kazi.
Viungo: Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Saidi Ntibanzonkiza, Luis Miquissone na Willy Essomba Onana.
Washambuliaji: Jean Baleke, Moses Phiri na Kibu Denis