MKAKATI wa zao la pamba uliowekwa mkoani Simiyu utauwezesha mkoa huo kuzalisha tani laki tano za pamba ambazo zitawezesha Tanzania kuwa kinara wa zao la pamba barani Afrika na hatimaye kuingia kumi bora duniani.
Hayo ameyasema Juma Topera ambaye ni katibu tawala msaidizi uchumi na uwezeshaji kutoka wilaya ya Meatu kwenye kikao cha kwanza cha tathimini ya zao hilo kilichofanyika wilayani Meatu mkoani humo.
“Tukizalisha tani laki tano ndani ya mkoa wetu tutawezesha nchi yetu kushika namba moja barani Afrika .. uzalishaji wa msimu 2019/20 nchi ya Burkinafaso ilikuwa ya kwanza kwa kuzalisha tan laki 265,500 ikifatiwa na nchi ya Mali kwa tan milioni 232,748 Nigeria tan laki 100,005, na Egypt tan laki 100,013 amesema Topera na kuongeza kuwa :
“Nchi ya India kwa msimu wa kilimo 2019/20 ndio iliongoza kwa kuzalisha tan milioni 6,178,000 ikifatia na China tan milioni 6,168,000 na marekani tan milioni 3,593,000 Algentina ilishika nafasi ya 9 kwa kuzalisha tan laki 327,000 na Uturuki nafasi ya 8 kw kuzalisha tan laki 846,000 hivyo mkoa wetu ukiweza kuzalisha tan laki tano tutaingia kumi bora duniani “ameongeza.
Akizungumza na wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika kikao chake cha kwanza cha tathimini ya zao hilo wilayani hapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila, amewataka wadau wote wanaohusika na zao hilo kila mmoja kutekeleza mikakati ili kufikia lengo.
Awali mkuu wa wilaya ya Meatu Fauzia Hamidu alisema tayari wameanza utekelezaji wa mikakati hiyo ikiwemo uhamasishaji .
Na Anita Balingilaki, Simiyu



























