Timu ya Singida Big Stars imetolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-1 na kutoka kwa klabu ya Modern Future katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 bora jana Jumapili jioni katika Uwanja wa WE Al-Ahly mjini Cairo nchini Misri.
Singida Big Stars inatolewa kwa kichapo cha jumla cha mabao 4-2 kufuatia ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.