SHIRIKA la Umeme Tanzania-TANESCO, limetia saini mkataba wa zaidi ya Shilingi Bilioni-69 na Kampuni ya Kimataifa ya Teknolojia ya India Tech Mahindra ili kusaidia kuboresha utoaji huduma kwa Mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande, amesema Jijini Dodoma kuwa Tech Mahindra imeshinda Zabuni ya kusaidia kubuni mfumo wa Mipango wa Rasilimali za Biashara ambao utasaidia Tanesco kutambua kwa haraka masuala yanayowaathiri wateja na wafanyakazi na kuyatatua kwa haraka.
Tanesco imesema mfumo huo mpya pia utapunguza gharama za kila siku zinazotumika wakati wa kutekeleza majukumu yake.
Mfumo huo mpya ni sehemu ya mkakati wa Kampuni wa kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma nchini.
Na MWANDISHI WETU



























