Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Rais Samia Suluhu
Hassan, ametoa maagizo ya kujengwa kampasi 14 katika mikoa ambayo haina vyuo vikuu ili
inufaike na elimu ya juu.
Profesa Mkenda alitoa maagizo hayo jana wakati akizindua kampeni ya ‘Niache nisome Pangani
inanitegemea’ iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Zainab Abdallah na
Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso, ambaye pia ni Waziri wa Maji.
Waziri Profesa Mkenda alisema Tanga kutajengwa kampasi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe
ambapo awali Waziri Aweso aliomba chuo kikuu kijengwe mkoani hapo ili kuwainua wananchi
kiuchumi kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka.