SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) limeingia mkataba wa kurusha matangazo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka 10 wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.54.
Mkataba huo unaipa TBC pekee haki ya kurusha matangazo kwa sauti, na chombo kingine kikitaka kurusha matangazo kwa sauti lazima kiwe na makubaliano na TBC.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, wakati wakisaini mkataba huo, jijini Dar Es Salaam.
Karia amesema: “haki ya urushaji wa matangazo ya mpira wa miguu kwa njia redio ipo kwa TBC, kwa vyombo vingine vya habari haviruhusiwi kurusha matangazo bila kupata kibali kutoka TBC.
Na Mwandishi wetu