Uhamisho wa kiungo wa kati wa Manchester City na England Kalvin Phillips, 28, kwenda Newcastle United unaweza usifanyike. Lakini Fulham na Crystal Palace wanavutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Leeds. (I Sport)
Manchester United wameandaa orodha ya wachezaji wanne ili kupata mshambuliaji mpya mwezi Januari, nao ni Mcameroon wa Bayern Munich, Eric Maxim Choupo-Moting, 34, mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 34. Klabu hiyo pia imewasiliana na RB Leipzig juu ya Timo Werner wa Ujerumani, 27, na mshambuliaji wa Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy, 27. (Athletic)
Mshambulizi wa Uingereza, Ivan Toney, 27, ana matumaini ya kuhamia Arsenal mwezi Januari lakini The Gunners hawana nia ya kulipa pauni milioni 100 ambayo Brentford wanataka. (Football Transfers)
Winga wa Manchester United na England, Jadon Sancho, 23, anatamani kurejea Borussia Dortmund. (Fabrizio Romano).
Tottenham hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza, Conor Gallagher, 23, mwezi Januari kwa sababu hawawezi kutimiza matakwa ya Chelsea ya pauni milioni 60 kutokana na vikwazo vya kifedha (Football Transfers)
Everton wanafikiria kumpa kiungo wa zamani wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard mkataba hadi mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa ni mchezaji huru. (Talksport).