BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hussein Itaba, ametamba kumchakaza mpinzani mwenzake, Ibrahim Tamba, katika pambano la ‘Usiku wa Nyodo’ utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi uliopo urafiki, Dar es Salaam.
Pambano hilo lenye mizunguko ‘raundi’ 10, uzani wa kilo 52, ambalo litawakutanisha wababe hao litafanyika Julai 17, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Itaba amesema anaendelea kujifua imara ili kushinda katika pambano hilo.
Itaba ameeleza kuwa anazingatia mazoezi anayofundishwa na kocha wake ili kupata matokeo mazuri.
“Lengo langu ni kupata ushindi, nawambia mpinzani wangu akae tayari kusubili makonde makali kutoka kwangu,” amesema Itaba.
Bondia huyo amesisitiza kuwa mazoezi anayoyafanya ni makali ambayo atahakikisha anawapa burudani mashabiki zakle.
“Mashabiki wangu wakae tayari kusubili ushindi kutoka kwangu, naamini watafurahi na kuburudika siku hiyo,” amesema Itaba.
Itaba ameeleza kuwa muda mwingi anautumia katika mazoezi ili kujifunza vitu vipya ambavyo vitampa ushindi.
Na AMINA KASHEBA