Waamuzi wawili wa soka nchini waliokuwa na beji ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Jonesia Rukyaa na Sudi Lila hawatachezesha tena mechi za kimataifa za Fifa na CAF baada ya kushindwa kurudia mtihani wa utimamu wa mwili (cooper test).
Kwa sasa waamuzi hao watapaswa kusubiri hadi Julai mwakani ambapo Fifa itafanya tena kozi ya na kama watakuwa na sifa stahiki, basi wataruhusiwa kushiriki kozi hiyo lakini watabaki kuchezesha mechi za ligi ya ndani.Jonesia na Sudi walifeli kozi hiyo iliyofanyika Agosti jijini Dar es Salaam ikisimamiwa na FIFA na walipaswa kurudia mtihani wa utimamu wa mwili Septemba, lakini inadaiwa hawakupeleka majina yao FIFA.
Wakati wawili hao wakishindwa, Tanzania imepeleka majina mawili ya waamuzi wa kike Fifa, Tatu Malogo na Amina Kyando ambao walifanya vizuri kwenye kozi hiyo ili kuwaombea beji ambazo hutolewa kila Januari ya mwaka unapoanza.