Na Godfrey Sanga (Uelekeo Gazeti)
ZAIDI ya mama na baba lishe 500 mkoani Njombe, wamepewa mitungi ya gesi kukabiliana na uharibifu
wa mazingira kwa kukata miti ovyo kwa ajili ya kuni na mkaa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi hiyo mwishoni mwa wiki, Mbunge wa Viti Maalum wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Neema Mgaya, alisema serikali imedhamiria kutoa elimu na nishati mbadala
ili wananchi waache kukata miti kwa lengo la kupata kuni na mkaa, hatua ambayo inaharibu mazingira.