WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani ili kutekeleza miradi ya maendeleo itakayotatua kero za wananchi.
Ummy aliyasema hayo leo, alipozungumza na Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani, alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Amesema hatasita kuwachukulia hatua Wakurugenzi watakaoshindwa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
“Tunakusanya ushuru wa mazao, ushuru kutoka kwa wafanyabishara wadogo, tunawatoza ushuru kupitia huduma, hivyo ni wajibu wetu kurudisha huduma kwa wananchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesisitiza Waziri Ummy

Amesema ni wajibu wao kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ambayo itatatua kero za wananchi ikiwemo afya, elimu na miundombinu ya barabara.
Aidha, ameziagiza Sekretarieti za Mikoa yote nchini, kuhakikisha zinasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri na fedha zinazokusanywa zitengwe kutekeleza miradi ya maendeleo.
Na Angela Msimbira (TAMISEMI), Pwani