Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 kwenda kuhakiki majina yaliyoandikishwa kwenye daftari hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Waziri Mchengerwa amesema orodha hiyo inabandikwa kuanzia leo katika sehemu za matangazo ya uchaguzi kwenye vijiji na mitaa ili kuwezesha wananchi kuomba kurekebisha majina, kubadilisha taarifa au kufuta jina iwapo aliyeorodheshwa amefariki dunia.