Watu 13 wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Ally’s lenye namba za usajili T.178 DVB lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda Jijini Mwanza baada ya kugonga Treni za mizigo maeneo ya Manyoni leo Novemba 29,2023 majira ya Saa 11 alfajiri.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk imesema “Ajali imehusisha basi la abiria lililokuwa likivuka njia ya reli eneo la Kilomita 587 Manyoni na kugonga kichwa cha treni na kusababisha Majeruhi 25 (Wanawake saba, Wanaume 18) pamoja naa vifo vya Watu 13 (Wanawake 6 na Wanaume 7).
“Shirika litaendelea kuutaarifu umma kadiri taarifa zinavyopatikana na linaendelea kuwasihi Madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria na alama za usalama katika njia ya reli na barabarani zilizowekwa ili kuepusha ajali, Shirika linatoa pole kwa Ndugu wa Marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi waweze kuendelea na shughuli za kujenga Taifa”
